12 Agosti 2025 - 22:27
Usafishaji Mkubwa wa Maficho ya ISIS katika Mikoa 4 ya Iraq

Kwa kushirikiana na Idara ya Kitaifa ya Ujasusi ya Iraq, maficho 10 na mitaro 3 imepekuliwa katika Kirkuk, huku pango moja la mawe katika mkoa wa Diyala likiharibiwa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Idara ya Kupambana na Ugaidi ya Iraq imetekeleza msururu wa operesheni za wakati mmoja na kuwakamata wanachama 11 wa kundi la kigaidi la ISIS, sambamba na kusafisha na kulipua mapango na mitaro kadhaa ya kundi hilo katika maeneo mbalimbali nchini Iraq.

Taarifa ya idara hiyo imesema kuwa hatua hizo zimefanyika katika muktadha wa operesheni kubwa zinazolenga kufuatilia mabaki ya magaidi wa ISIS kama sehemu ya juhudi za kitaifa za kudumu za kuutokomeza ugaidi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo:

Magaidi 5 wamekamatwa katika mkoa wa Nainawa, Wanne katika Mkoa wa Kirkuk, Mmoja katika mkoa wa Salahuddin, na mwingine mmoja katika Mkoa wa Sulaymaniyah.

Aidha, kwa kushirikiana na Idara ya Kitaifa ya Ujasusi ya Iraq, maficho 10 na mitaro 3 imepekuliwa katika Kirkuk, huku pango moja la mawe katika mkoa wa Diyala likiharibiwa.

Operesheni hizo zimefanyika kwa mujibu wa maagizo ya kisheria yaliyotolewa na mahakama ya Iraq, ambapo kwa kufuata taarifa za kijasusi kwa umakini, vikosi vya kupambana na ugaidi vimefanikisha mashambulizi ya awali ili kumaliza kabisa uwepo wa ISIS nchini humo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha